MTAZAMO WA SEKTA YA KILIMO KWA VIJANA AFRIKA
Vizazi vinabadilika na kupita lakini mahitaji ya bidhaa za mazao ya kilimo yanaongezeka kila siku.
Toka zamani na mpaka sasa kwa kiasi kikubwa mkulima amekua akionekana kwa picha ya mazoea kuwa ni mzee mmoja, mwenye jembe lake mkononi, mwenye kikapu cha muhogo au viazi, nguo zake zikiwa zimejaa vumbi na tope akipita katika kingo za barabara akirudi nyumbani kwake ambapo hakuna umeme na nyumba yake yenye umbali wa kilometa zaidi ya 4.5 kutoka shambani iliyoezekwa na majani makavu. Hii ni picha ya "mkulima" iliyoko katika akili za watu wengi.
Kama leo ukimchukua mtoto wa darasa la 6 ukimwambia achore picha ya mkulima nafkiri atakuchorea mtu mwenye muonekano kama huo. Lakini dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana(Ruge Mutahaba, CloudsMediaGroup); mabadiliko ya dunia katika nchi hasa zinazoendelea ni lazima yaende na mabadiliko ya fikra na muonekano wa tafsiri ya neno maendeleo katika fikra za watu.
Ukuaji wa Sayansi na teknologia umeleta mabadiliko makubwa sana, hasa katika kusaidia sekta mbalimbali kukua katika utoaji huduma kwenye jamii mbalimbali. Mabadiliko haya lazima yaende sambamba na mabadiliko ya kimtazamo katika sekta mbalimbali. Katika sekta ya kilimo barani afrika, ambayo kiutafiti inaweza kutengeneza ajira zaidi ya Milioni 25 kwa vijana hadi mwaka 2050, matumaini ya vijana kuhamasika katika uwekezaji wa sekta ya kilimo bado ni madogo sana. Hii inatokana na mtazamo wa kifikra walionao kwenye sekta ya kilimo.
Zipo sababu nyingi zinazowafanya vijana wasiione fursa hii; mojawapo ikiwemo mtazamo hasi wa sekta ya kilimo. Vijana wengi wamekulia katika shule ambazo adhabu kubwa ni kupelekwa kulima shambani na hata muonekano wa mkulima haumvutii kijana kutokana na picha ya zamani ya kila mkulima. IPO KAZI YA KUFANYA HAPA.
Kwanza si kila kijana anaweza kuingia katika uwekezaji katika kilimo lakini ndio sekta inayopewa nafasi kubwa duniani katika kutengeneza ajira na kipato kwa vijana, ni sekta inayohitaji nguvu kazi kubwa ambayo inapatikana kwa vijana, ni sekta ambayo uwekezaji wake kwa kiwango cha awali si mkubwa, na kubwa zaidi ni sekta yenye soko la uhakika kulingana na mahitaji. Kwa wale wenye matazamio na nia ya kuwekeza, hawana budi kuanza kwanza kutazama uwekezaji katika sekta ya kilimo kibiashara zaidi. Kijana aone kilimo kama biashara sawa na biashara nyingine ambazo zinaweza kumuingizia kipato na faida kubwa na kuweza kuendesha maisha yake vizuri.
Hivyo mabadiliko ya kisekta katika bidhaa na wasifu(Agricultural re-branding) yanahitajika. Taasisi husika zilizopo kwenye sekta ya kilimo lazima zijikite katika kuleta mageuzi ya kifikra hasa kwa vijana kuhusu fursa za sekta ya kilimo. Hapa kuna maeneo mawili(2) muhimu ya kuangalia, (1) Jambo la kwanza ni kutazama sekta ya kilimo Kibiashara (2) Tumtafsiri mkulima kama mjasiliamali na si mkulima tuu, hivyo anapaswa kuitwa mjasiliamali wa kilimo(Agri-preneur).
Mabadiliko ya ubora wa bidhaa na soko katika sekta ya kilimo hayawezi kufanikiwa kama hatutaanza kumtazama mdau wa kwanza kabisa ambae ni mzalishaji wa mazao shambani, kama mjasiliamali na si tuu mkulima. Ukimtambua mkulima kama mjasiliamali wa kilimo na kushirikiana nae kibiashara ni vema zaidi, kuliko kumchukulia kama mkulima wa kawaida tuu.
ITAENDELEA WIKI IJAYO
ASANTE SANA
Na:
Daniel Kapinga(MBA-Agribusiness)
Kilimo Forum

Mabadiliko lazima yaanzie hapa
ITAENDELEA WIKI IJAYO
ASANTE SANA
Na:
Daniel Kapinga(MBA-Agribusiness)
Kilimo Forum

No comments