Muendelezo wa Mkutano wa #AGRF

Mkutano mkuu wa mapinduzi ya kijani barani afrika yaani Africa Green Revolution Forum(AGRF) umeendelea jana na leo mjini Abidjan, nchini Ivory Coast, huku mada mbalimbali, mikutano na midahalo inayo washirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo barani afrika ikifanyika.

Moja ya mada zilizojadiliwa kutoka jana na leo ni pamoja na uwekezaji wa kifedha katika kutekeleza mapinduzi ya sekta ya kilimo barani afrika, kuwezesha ugunduzi(uvumbuzi) katika sekta ya kilimo barani afrika, ushiriki wa vijana katika ugunduzi na uvumbuzi wa teknologia mbalimbali zinazogusa sekta ya kilimo barani afrika.

Rais mstaafu wa Tanzania, Mh Dk Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja ya washiriki wa mkutano huo, amewasilisha ripoti ya hali ya lishe barani afrika katika mkutano huo, huku tafiti zikionyesha wawekezaji wameonyesha nia ya kuwekeza katika kilimo kama sekta iliyoshika nafasi ya pili katika uwekezaji barani afrika. Pia udhibiti wa wadudu waharibifu ni moja ya mada zilizojadiliwa huku taarifa kwa wadau wakiwemo wakulima kuhusu dalili na athari za wadudu hao zikipewa kipao mbele.

Pia katika mfululizo wa mkutano huo, vijana mbalimbali kutoka nchi za afrika walipata fursa ya kushirikiana na wadau kueleza mawazo yao katika ubunifu mbalimbali kusaidia kuinua sekta ya kilimo barani afrika.

Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio ya muendelezo wa mkutano huo:








No comments

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.