Wadau wa korosho nchini wakutana mkoani Tanga

Kikao cha kamati zinazohusisha vyama vikuu vya ushirika, washauri wa kilimo kutoka mikoani na wawakilishi 5 kutoka mikoa inayolima zaidi zao la korosho na wawakilishi kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele; wamekutana mkoani Tanga kujadili mchakato wa ununuzi wa zao na upandaji wa bei elekezi ya zao la korosho kwa mwaka 2017/18. Kaimu mkurugenzi wa bodi ya korosho; Bwana Hassan Jarufu amesema maandalizi ya ununuzi wa zao la korosho umeshakamilika.



Nae mwenyekiti wa Bodi ya korosho nchini; mama Anna Abdala amesema bei ya zao la korosho mwaka huu itapanda kutoka 1,300Tsh kwa kilo hadi 1,450Tsh huku makato yakiwa 143Tsh. Wakuu wa wilaya za Tunduru na Namtumbo zinazozalisha korosho kwa wingi; wamewaagiza wakulima kuachana na mfumo wa ununuzi wa korosho kwa njia ya ulanguzi, na badala yake watumie mfumo wa bei elekezi ambao utakua na tija kwa wakulima.


No comments

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.