BILL GATES ATOA US$350M KUSAIDIA SEKTA MBALIMBALI IKIWEMO KILIMO
Mfanyabiashara tajiri kutoka marekani Bill Gates ambae pia
ni mwenyekiti wa Bill & Melinda Gates, amefanya mazungumzo rasmi na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli ikulu jijini Dar es
salaam leo. Katika mazungumzo hayo;moja ya maafikiano yaliyofikiwa ni kutoa fedha kiasi cha Dola
za marekani US$350 Milioni(Zaidi ya Bilioni 777) kwa ajili ya kuwezesha
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo kilimo.
Katika sekta ya kilimo ambayo kiasi kikubwa cha fedha hizo
kitatolewa kulenga miradi ya maendeleo ya kilimo; Bwana Gates ameeleza dhamira
yake ya kutoa fedha hizo kupitia taasisi ya Bill and Melinda Gates foundation
ni kusaidia uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya kilimo na kuongeza uzalishaji
mashambani.

No comments