WAKULIMA 30,000 UPATA MICHE YA CHIKICHI
Takribani wakulima 30,000
mkoani Kigoma watafaidika na hatua ya Taasisi kuinua na kusaidia sekta binafsi (PASS)
kuanzisha hatua ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara kwa kipindi cha
miaka mitatu(3). Manager wa PASS mkoa wa Kigoma bwana Faustine Mungo, akiongea
na waandishi wa habari amesema wakulima hao watafaidika kwa kupata mbegu za zao
la chikichi chini ya taasisi za kijamii ya Seed Change Tanzania(SCT) ambayo
imepata fedha kutoka PASS.
Bwana Mungo amesema
SCT imefanikiwa kuingiza miche ya mbegu za chikichi zaidi ya 60,000 kutoka Costa
Rica ambayo itagawiwa kwa wakulima hadi mwisho wa mwaka huu. Amesisitiza kuwa
lengo lilikua kuwafikia wakulima 10,000 kabla ya mwisho wa mwaka huu. PASS
imefanikiwa kuwasaidia wakulima kupitia miradi mbalimbali yenye thamani ya
Bilioni 13.2 katika kanda ya magharibi yenye inayohudumia mikoa (3) ambayo ni
Tabora, Kigoma na Katavi.

No comments