MBEGU MPYA YA ZAO LA ALIZETI YAZALISHWA



Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Joel bendera amewaagiza wakulima mkoani humo kutumia mbegu mpya za alizeti zilizozalishwa hivi karibuni zenye ubora na uzalishaji unaofikia gunia 18-25 kwa ekari zaidi ukilinganisha na mbegu za sasa zinazozalisha kiasi cha magunia 5-7 kwa ekari.




Akiwasilisha agizo hilo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara; Mkuu wa wilaya ya Babati Mh. Raymond Mushi kwa wakulima na wadau wa kilimo, wakati wa uzinduzi wa mpango wa kilimo biashara na mifumo ya masoko kupitia mbegu mpya utakaotekelezwa ndani ya miaka 5. Mpango huo unaosimamiwa na nchi 4 yaani Denmark, Sweden, Uswizi na Ireland utawahusisha wakulima katika wilaya ya Babati, Hanan, Mbulu na Simanjiro.

No comments

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.