Serikali kuagiza Tani 55,000 za Mbolea
Serikali chini ya Wizara ya kilimo inatazamia kuagiza mbolea ya kukuzia na kupandia takribani tani 55,000 kupitia mfumo mpya wa kuagiza mbolea kwa pamoja. Hatua hii inakuja baada ya kupanda kwa bei za mbolea nchini jambo ambalo wakulima nchini wanashindwa kumudu bei hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya kudhibiti ubora wa mbolea chini ya Wizara ya kilimo(TFRA), Lazaro Kitandu amesema hatua hiyo inakuja baada ya bei za mbolea kupanda nchini. Bwana Kitandu amesisitiza kuwa kama wizara imefanya tathmini ya miaka 5 inayoonyesha kila baada ya miezi 2 serikali inahitaji kiasi gani cha mbolea.
Bwana kitandu amesema mbolea hizo zitaanza kuingia nchini september 5-15 mwaka huu kupitia kampuni mbili za OCPSA ya nchini morocco na PREMIUM AGRO CHEM ya hapa nchini ambazo zilishinda zabuni za kuingiza mbolea nchini.

No comments