Kilele cha maonyesho ya Kilimo 88.
Kilele cha maonyesho ya wakulima 88 ni leo tarehe 08/08/2017.
Kauli mbiu ya maonyesho ni "Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati"
Dhumuni kubwa la maonyesho haya ni kuonyesha kazi mbalimbali za uzalishaji katika sekta ya kilimo zilizo chini ya taasisi za serikali na binafsi na kutoa nafasi kwa wakulima na watu mbalimbali kukutana na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo nchini.
Maonyesho haya kitaifa yatafanyika mkoani Lindi ambapo Makamu wa Rais, Mh Samia Suluhu Hassan atakua mgeni rasmi.
Tunawatakia sikukuu njema ya wakulima.

No comments