Hati 2,111 vya umiliki wa ardhi kutolewa Kilombero

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi chini ya programu ya matumizi bora ya ardhi, wiki ijayo inatarajia kutoa hati zaidi ya 2,000 za umiliki wa ardhi katika kijiji cha Nyange wilayani kilombero, mkoani Morogoro.



Zoezi hilo litaanza mkoani Morogoro siku ya jumanne, ambalo litasimamiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi Mh Willium Lukuvi ambapo zaidi ya hati za umiliki 2,111 zitagawiwa kwa wanakijiji hao. Zoezi hilo linafanyika kufuatana na utaratibu wa serikali kuhakikisha matumizi bora ya ardhi yanazingatiwa na watumiaji wote wa ardhi nchini.

Zoezi hili pia limegusa wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero ambao pia watafaidika na mradi huu. Katika zoezi hilo zaidi ya mashamba 21,154 yamepimwa katika wilaya ya Kilombero na Ulanga ikiambatana na upimaji wa mipaka 50 iliyosaidia kumaliza migogoro 18 ya mipakani katika vijiji husika.

Programu hii ya miaka 3 inayosimamiwa na Wizara ya ardhi, inatazamiwa kugharimu kiasi cha Dola za marekani 15.2 Milioni(Bilioni 34 za Tanzania) fedha zilizotoka kwenye mifuko ya DFID kutoka Uingereza, SIDA(Sweden) na DANIDA(Denmark).

No comments

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.