Wakulima tumieni mbegu zinazostahimili Ukame

Katika maonyesho ya kilimo (88) ambayo yako kwenye siku ya tatu leo(Trh 3/8/2017) katika viwanja mbalimbali mkoani Arusha, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Lindi; wakulima wamepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali na kupokea ushauri kwa wadau mbalimbali wa kilimo nchini wakiwemo wataalam kutoka taasisi za kiserikali na zile za binafsi zikiwemo kampuni mbalimbali.

Moja ya ushauri mkubwa kwa wakulima katika mwaka huu wa maonyesho ni matumizi ya mbegu bora na hasa zinazostahimili ukame katika kanda mbalimbali za kilimo nchini. Kilimo Forum(KF) imefanya mahojiano na moja ya kampuni zinazozalisha mbegu aina chotara ya mahindi ya manjano (CP-201).


Moja ya sifa za mbegu hii:

1. Inastahimili ukame
2. Uzalishaji ni gunia 20-30 gunia/ekari
3. Ina vitamin A(Carotene) na Protein




No comments

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.