MKURUGENZI WA FAO KUFANYA ZIARA NCHINI TANZANIA
Mkurugenzi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani(FAO) Jose Graziano Da Silva anatarajia kuanza ziara yake nchini Tanzania leo Jumanne ambapo atakutana na kufanya vikao na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kilimo ikiwemo serikali.
![]() |
| Mkurugenzi wa FAO; Jose Graziano Da Silva |
Katika ziara hiyo, Bwana Da Silva atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Dr John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein. Baada ya hapo Bwana Da Silva atakutana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dr Charles Tizeba na Hamad rashid Mohammed wa Zanzibar.
Ujio wa Mkurugenzi wa FAO Tanzania unakuja katika kutimiza miaka 40 ya FAO kufanya kazi nchini Tanzania. Sambamba na hayo ujio wa Bwana Da Silva utaambatana na maongezi ya kina baina ya FAO na Tanzania katika kuimarisha usalama wa chakula nchini. Ziara hiyo itasitishwa kwa Bwana Da Silva kutembelea zanzibar na kuweka jiwe la msingi la mradi wa uzalishaji wa samaki uliojengwa chini ya serikali ya watu wa Korea.

No comments