Mradi mpya wa PIATA kuwekeza US$280M kwenye Kilimo Afrika Mashariki
Nchi za
afrika mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya, Ethiopia na Rwanda zitafaidika na
program ya uwekezaji wa kifedha kwenye kilimo, yenye lengo la kuongeza kipato
na usalama wa chakula kwa familia zaidi ya milioni 30 katika nchi 11 barani
afrika mpaka mwaka 2021. Program hiyo ya Partnership for Inclusive Agricultural
Transformation in Africa (PIATA), inatazamia kutoa kiasi cha Dola za kimarekani
Milioni 280(US$280 Million) katika kuleta mapinduzi ya kilimo barani afrika.
![]() |
| Partnership for Inclusive Agricultural Transformation in Africa |
![]() |
| Bill & Melinda Gates Foundation |
Mkurugenzi mtendaji wa Rockerfeller Foundation, bwana Mamadou
Biteye, amesema ushiriki huo utasaidia wadau hao kusaidia maendeleo ya afrika
na uwezeshaji kwa wananchi kuwa mkubwa kupitia mapinduzi ya sekta ya kilimo
barani humo. "Tunategemea kupeka teknologia ambazo zitasaidia sekta ya
kilimo kwa miaka kadhaa ijayo, kukusanya mawazo yetu na uzoefu ambao utasaidia
kuwafikia watu wengi zaidi”
![]() |
| Mkurugenzi mtendaji wa Rockerfeller Foundation, bwana Mamadou Biteye |
Kuanzishwa
kwa mradi huo kutasaidia malengo ya Azimio la Maputo la mwaka 2014 la
kuhamasisha uwekezaji wa kifedha kwenye sekta ya kilimo barani afrika. Nae
bwana Sean Jones, mwakilishi kutoka USAID amesema PIATA itasaidia kuja na njia
mpya ya kufanya biashara na kuhakikisha usalama wa chakula na ukuaji wa uchumi wa
nchi husika.
![]() |
| Raisi wa Alliance for a Green Revolution in Africa, Bi Agnes Kalibata |
Nae Agnes Kalibata, Rais wa Alliance for a Green Revolution in Africa, amesema uhusiano huo wa washiriki utasaidia sana ukuaji wa nchi husika na kutengeneza ajira kupitia sekta ya kilimo, kusaidia serikali kuwezesha wakulima wadogo wadogo na ukuaji wa kilimo biashara. Ghana, Mali, Burkina Faso, Malawi na Msumbiji ni baadhi ya nchi ambazo pia zimeingia katika mpango huo.




No comments