LAPF yasaini mkataba wa Bilioni 10 kujenga kiwanda Mvomero
Mfuko wa mafao wa LAPF umesaini mkataba wa ubia na kampuni ya Eclipse Investment Limited ya Oman kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyama na machinjio ya kisasa katika wilaya ya mvomero mkoani Morogoro. Katika mkataba huo uliosainiwa hivi karibuni, zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 10 sawa na 39% ya umiliki kwa ajili ya ujenzi wa machinjio hayo zimetolewa na LAPF, mkataba uliosainiwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Stephen Kebwe na Katibu Tawala wa Mkoa Clifford Tandari.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Eliud Sanga amesema hatua hiyo ya ubia wa ujenzi wa kiwanda na machinjio hayo yatakayojengwa chini ya ranchi ya Nguru Hill ni fursa nzuri kwa taasisi ya mafao kama LAPF katika kuungana na azma ya serikali ya awamu ya 5 ya kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati. Ameendelea kusema kuwa uwekezaji wa machinjio ya Nguru Hill ni hatua ya awali tuu ya LAPF kuwekeza katika sekta ya viwanda na kwa mkoa wa Morogoro ni uwekezaji wa 2 mkubwa baada ya ule wa kwanza wa Stendi kuu ya mabasi Msamvu, Morogoro.
Bwana Sanga ameendelea kusema kuwa katika hatua ya awali fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa miundombinu ya machinjio hayo na ununuzi wa magari ya kusafirisha nyama. Pia ameeleza kuwa mradi huo una faida kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafugaji, kuzalisha ajira, kufaidika na soko la nje la nyama hasa kutoka Oman.

No comments