FAO kusaidia Tanzania katika Kilimo na Viwanda

Mkurugenzi wa shirika la Chakula na Kilimo duniani(FAO); ndugu Jose G. Da Silva katika ziara yake nchini Tanzania amesema kuwa FAO itasaidia Tanzania katika kuinua uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini na ufunguzi wa viwanda.


Akiongea na mwenyeji wake; Rais wa Tanzania Dr. John P.J Magufuli ikulu jijini Dar es salaam; bwana Da Silva alimshukuru Mh. Rais kwa juhudi za nchi katika ushirikiano baina yake na FAO uliodumu miaka 40 mpaka sasa. Amesema Tanzania inaweza kunufaika kwa kiasi kikubwa katika kuongeza uzalishaji wa chakula, uzalishaji wa ajira, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na ongezeko la pato la taifa kupitia kilimo na viwanda vya nyama na samaki.


Nae Rais wa Tanzania Mh Dr John P.J Magufuli amesema Tanzania itaendeleza ushirikiano wake na FAO ili kuhakikisha mipango yote ya kimaendeleo baina ya FAO na Tanzania inakamilika. Mh Rais ameendelea kusema kuwa Tanzania kwa sasa inakua kiuchumi kwa asilimia 7.1, tuna ukanda wa bahari wenye urefu wa 1422 km, ambao utasaidia kuazisha viwanda vya kusindika nyama ya samaki, na takribani asilimia 75% ya idadi ya watu wake ni vijana, ambao wanaweza kufaidika na ajira zinazopatikana kupitia sekta ya kilimo.



No comments

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.