MKUTANO WA AGRF WASITISHWA LEO.

Mkutano wa Africa Green Revolution Forum(AGRF) umemalizika leo mjini Abidjan, nchini Ivory Coast leo. Moja ya mambo yaliyofanyika katika siku 2 za mwisho za mkutano ni ugawaji wa zawadi za mawazo mazuri ya kiubunifu kwa vijana katika kilimo, Utoaji wa tuzo ya #AfricanFoodPrice, maendeleo na mchango wa teknologia katika kilimo(Mf. Teknologia ya ndege zisizo na abiria maarufu kama Drones) na ushiriki wa vijana kwenye mapinduzi ya kilimo barani Afrika.

Tuzo zilizotolewa ni ile ya Africa Food prize ambapo Prof Ruth Khasaya Oniang'O na Mrs Maimouna Sidile wakati zile za vijana zimeenda kwa kampuni ya teknologia ya kilimo ya AgroCenta na FarmAtGhana kampuni ya kuuza mboga mboga na matunda mtandaoni kutoka Ghana. Uwekezaji wa teknologia umeendelea kuhimizwa katika kilimo na uhamasishaji wa vijana katika ushiriki wa uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Nae Rais wa AGRF Dr. Agnes Kalibata amesisitiza ushiriki wa vijana na kuwekeza katika juhudi za vijana kwenye mapinduzi ya kilimo barani Afrika.

Zifuatazo ni Picha za matukio mbalimbali ya hitimisho la mkutano huo.






No comments

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.