MRADI WA FEED AFRICA STRATEGY WATENGEWA US$24B

Viongozi mbalimbali barani afrika na wadau katika sekta ya kilimo wameupongeza mradi wa Feed Africa Strategy ambao uko chini ya Benki ya maendeleo Afrika(AfDB) kama mkakati pekee wa kuleta mapinduzi katika sekta ya chakula na kilimo. Mradi huo wa miaka 10 unaosimamiwa na Benki ya maendeleo afrika umetengewa kiasi cha Dola za Marekani 24 Bilioni. Mradi huo ulioanza mwaka 2016 ulipangiwa Dola za marekani 30 Bilioni katika uwekezaji wa kuzalisha, kukuza kipato na kutengeneza ajira na kuwezesha wakulima wadogo.

"Maendeleo ya kilimo yakienda vizuri, kila kitu kitaenda vizuri. Tunahitaji sana wadau zaidi katika program hii" amesema Rais Ouattara wa Ivory Coast akifungua mkutano wa Mapinduzi ya kijani barani afrika mapema mwezi huu. Nae Rais wa AGRA Agnes Kalibata amesema kwa mwaka huu(2017) mradi wa Feed Africa strategy utalenga kuwezesha wakulima wadogo kutengeneza ajira nyingi na chakula cha kutosha barani afrika, lazima tuwekeze nguvu nyingi na kuhakikisha mipango yetu inasonga mbele. Pia Agnes Kaibata amewaomba wadau mbalimbali kusaidia vijana kuwa wajasiliamali wa kilimo wazuri katika ukuaji wa uchumi wa afrika.

Lengo kuu la Mradi wa Feed Africa Strategy ni kuondoa umaskini barani afrika, kuondoa tatizo la njaa na lishe duni, kuifanya afrika kuwa muuzaji mkubwa wa chakula nje ya bara na kuifanya afrika kuongoza katika soko la dunia la mnyororo wa thamani hadi mwaka 2025.


Feed Africa Strategy
Link:https://www.afdb.org/fileadmin/uploads/afdb/Documents/Generic-Documents/Feed_Africa-_Strategy_for_Agricultural_Transformation_in_Africa_2016-2025.pdf

No comments

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.