MIFUKO YA NSSF NA PPF IMEWEKEZA KATIKA MIRADI YA SUKARI
Mifuko 2
ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF imewekeza katika kilimo na uzalishaji wa sukari nchini katika hatua ya kupunguza uhaba wa sukari sokoni. Mifuko hiyo imewekeza katika miradi
mikubwa 3 ambayo ni ule wa shamba la Mbigiri lenye ekari 120,000 na shamba la
mkulazi lenye ekari 63,000 na shamba la Mkulazi II ambalo nipo kiwanda cha
kuzalisha sukari kitakuwepo ambacho kitaweza kuzalisha kiasi cha Tani 250,000
za sukari kwa mwaka.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Charles Mwijage amesema
kwa mwaka Tanzania inatumia Tani 600,000 za sukari ambazo zaidi ya Tani 420,000 zinatumiwa kwa matumizi ya kawaida na iliyobaki ni kwa matumizi ya viwandani, wakati viwanda vya ndani
vya Kilombero, Kagera, TPC na Mtibwa wanazalisha Tani 290,000 kwa mwaka jambo
ambalo linalazimu nchi kuagiza sukari kutoka nje. Kwa mujibu wa bodi ya sukari
nchini, mwaka jana uzalishaji wa viwanda vya ndani ulikua ni Tani 290,112 tuu.
Nae
Mkurugenzi mkuu wa NSSF Prof Godius Kahyarara
amesema tayari mkandarasi wa ujenzi wa kiwanda ameshapatikana na hadi mwezi disemba
lengo kuu ni kupanda zao la miwa kwenye ekari 3,000 ambalo litatengeneza ajira
150 kwa wenyeji.


No comments