WAFUGAJI SIMANJIRO WAANZISHA MASHAMBA YA NYASI

Wafugaji kutoka wilaya ya simanjiro wameanzisha mashamba ya nyasi kwa ajili ya ulishaji wa mifugo na kuiomba serikali kuwapatia maeneo ya ardhi ambayo hayaendelezwi kwa ajili ya kuendeleza uzalishaji wa nyasi. Wafugaji wilayani humo wamesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali la kubadili mfumo wa ufugaji na kuboresha maeneo ya malisho ya mifugo ambao utasaidia kupunguza na kuondoa migogoro baina ya wafugaji na wakulima.




Mbunge wa Simanjiro Mh. James Ole Milia amesema hatua hiyo ni mwanzo mzuri na ukombozi kwa wafugaji na itawasaidia kuweka akiba ya malisho, kuongeza uzalishaji wa bidhaa za mifugo na kuongeza ubora wake pia, na kufuga kwa tija. Mkakati huo ukifanikiwa utakua mfano wa kuigwa kwa wafugaji katika maeneo mengine nchini.

1 comment:

  1. Enter your comment...bigup honorable milia,we support you all the way from Kenya

    ReplyDelete

Theme images by Xaviarnau. Powered by Blogger.